Tuesday, 10 December 2013

KANISA LATOA TAMKO:MANDELA YUKO JEHANAMU NA SIO MBINGUNI

Kanisa linalojulikana kama Westboro Baptist Church nchini uingereza limetoa tamko ambalo limeishtua dunia.

Limetangaza wazi kwamba Muasisi wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Mandela HAJAENDA MBINGUNI BALI ANAUNGUA NA MOTO WA JEHANAMU sasa hivi


Wametoa Ushahidi wa kusapoti tamko lao kwa sababu za UZINZI na wamesema wazi Mandela alioa Ndoa ya Kikristo kwa mkewe wa kwanza EVELYN lakini baadae alimuacha na kuoa isivyo halali mke mwingine aitwaye WINNIE ambaye naye aliachwa na kumuoa GRACA MACHEL, mke wa mjane wa Taifa la Msumbiji, SAMORA MACHEL


Kwa Mujibu wa Ndoa za Kikristo,Ukimuacha Mkeo na kuoa mke mwingine wakati mkeo yu hai UNAZINI


EVELYN, ambaye ni mke wa kwanza na wa halali wa HAYATI NELSON MANDELA alimzalia Nelson watoto wawili wa kiume ambao wote wameshakufa,Mmoja kwa Ajali ya Gari na mwingine kwa UKIMWI


Kanisa la Westboro wameshutumu vikali Mazishi ya Mandela na kusema yamejaa upotoshaji mkubwa wakishangaa kwanini azikwe mazishi ya kitakatifu wakati ameishi maisha ya Uchafu maisha yake yote


Tamko hili limetamka wazi kabisa kwamba kwa sasa MANDELA yuko Jehanum na anapewa kampani na watu wengine mashuhuri ambao wametajwa kuwa kwenye listi ya watu walio JEHANAMU wakiongozwa na STEVE JOBS(Muasisi wa Apple), MATTHEW SHEPHERD,JOHN LENNON,WHITNEY HOUSTON,LOU REED na GHANDI


Sikiliza na Angalia Video hii ambayo Mchungaji wa Kanisa hilo ameelezea kwa Undani kwanini MANDELA yuko JEHANAMu na sio MBINGUNI kama watu wanavyodhani

Bonyeza hapa kutazama http://www.youtube.com/watch?v=dd-gPRIvcTs


Thursday, 21 November 2013

MWANAMUZIKI WA FM ACADEMIA AUAWA NCHINI CHINA BAADA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Mwanamziki aliyepata kutamba na Bendi ya FM Academia ya jijini Dar es Salaam, Rapa, Haristot Shungu ameuawa nchini China huku kifo chake kikitawaliwa na utata mkubwa. 


Kwa mujibu wa chanzo  makini kilichopo nchini China, rapa huyo alikamatwa uwanja wa ndege baada ya kugundulika kuwa amebeba madawa ya kulevya akiwa ameambatana na rapa mwingine wa Bendi ya Akudo Impact, Kanal Top na wote wawili kuhifadhiwa mahabusu.
“Tulijua kama Haristot alikamatwa pamoja na Kanal Top lakini ghafla juzi (Ijumaa) tukaambiwa kuwa amefariki dunia, hatujui kifo chake kimesababishwa na nini lakini mwili wake unaonekana kama vile aliungua na moto au mtu aliyechomwa sindano ya sumu,” kimesema chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu aliwasiliana  na Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat na kumuuliza kama alikuwa na taarifa zaidi za Haristot.
Nyoshi alikiri kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki wao na kudai kwamba kifo chake kimetawaliwa na utata mkubwa.
“Haristot alikuwa mwanamuziki wetu, mara ya mwisho aliaga kuwa anakwenda Ulaya kwa mchumba wake, nimeshangaa kusikia ameuawa nchini China kiukweli hakuna anayejua ukweli wa kifo chake,” alisema Nyoshi.

Monday, 18 November 2013

RAISI AJAYE LAZIMA ATOKE KIGOMA...KAFULILA ANENA

Anaitwa David Kafulila,Mmoja kati ya Wabunge wenye umri mdogo na machachari sana kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ametoa Kauli yake kuhusu kumuunga mkono ZITTO KABWE kuwa Raisi wa Tanzania ifikapo mwaka 2015

''Naweka kumbukumbu sawa, mwaka 2012 kwenye tamasha la LEKA DUTIGITE kule Kigoma, wabunge Halima Mdee, Joshua Nassari na wengine wengi walijumuika na Zitto kwenye tamasha lile, walitoa kauli majukwaani wakimuunga mkono Zitto kuwa ndiye rais ajaye 2015'' Baada ya kauli zao walikutana na hali iliyotushangaza wengi na baadae walikana kutamka kumuunga mkono Zitto kwa suala hilo.


 Davidi kafulila mbunge wa kigoma kusini aliamua kuvunja ukimya na kuwatolea uvivu na kuanika waliyoyasema kwa picha na sauti zao.


HAPA NAMNUKUU " huu mjadala watu kukana hauna maana kabisa. wote wanaokana ndio wapiga debe wakubwa. waliyasema haya wanayoyakana. ni unafiki ndio unaowasumbua na uoga. kabla ya kuondoka, wote tulikaa pale sinza na kwa pamoja wakasema wanamuunga mkono, tukafika Kigoma wakarudia maeno yale yale ya kumuunga zitto. Iweje leo wanakana? Asilimia 85% ya wabunge wanamuunga mkono zitto kugombea urais. Wana kigoma tumeonewa sana. Muda umefika kuwepo usawa katika uongozi wa hii nchi. 

Hatuwezi kuwa wasindikizaji siku zote, wakati uwezo tunao. Tunaungwa mkono kila kona ya nchi na hata nje ya nchi, na kama ni demokrasia 2015 rais na makamu wake lazima watokee Kigoma. Rais wa Tanzania, Afrika Kusini, ujerumani na Malaysia wote wanataka umuona rais kijana Tanzania.Vyama vyote vya siasa humu nchini wanamtaka rais kijana, Kikwete mwenyewe anamtaka atakayemrithi awe kijana"

KAJALA KURUDISHWA JELA?MME WAKE AMKATIA RUFAA..HUKUMU KURUDIWA UPYA

Mwanadada Kajala Masanja ambaye miezi michache nyuma alifanikiwa kuepuka kifungo Jela baada ya Mwanadada Wema Sepetu kujitolea kumlipia dhamana ya Shilingi Milioni 13 sasa yuko hatihati kurudishwa Jela baada ya Mume wake kukata Rufaa dhidi ya Hukumu iliyomuachia huru



Tarehe 25 Mwezi Huu wa Novemba Kesi ya Kajala itatajwa upya Mahakamani na Hukumu itasomwa Upya kujua kama kweli Kajala ataendelea kubakia Uraiani au atahukumiwa kwenda Jela.
Macho na Masikio ya Watanzania wengi yameelekezwa tarehe hii kujua hatma ya Mwanadada huyu ambaye aliponea chupuchupu kuozea Jela kabla ya kuokolewa na Madam Wema aka In my Shoes Lady

Thursday, 14 November 2013

UTATA WAGUBIKA KIFO CHA DOKTA MVUNGI:MADAKTARI WATOFAUTIANA

Hospitali ya Millpark ya Johannesburg, Afrika Kusini, imesema madaktari waliokuwa wakimtibu aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi walibaini kuharibika kwa ubongo wake kutokana na kumwagika kwa maji yanayoutunza ambayo kitaalamu yanaitwa ‘cerebrospinal fluids’ au CCF.


Msemaji wa Hospitali hiyo, Tebogo Nyembezi alisema Dk Mvungi alicheleweshewa tiba baada ya kupata tatizo la maji hayo yanayotunza ubongo kumwagika mara baada ya kujeruhiwa.
Dk Mvungi (61), alipata majeraha makubwa baada ya kujeruhiwa na watu waliovamia nyumbani kwake Kibamba, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Novemba 3 mwaka huu. Alifariki dunia jana mchana.


“Maji hayo ambayo ni miligramu 50 tu katika ubongo wa mwanadamu ambayo huufanya ubongo uelee yakimwagika nusu tu, basi mgonjwa yupo hatarini, lakini akiwahishwa na kupata tiba sahihi anaweza kupona,” alisema Nyembezi.


Alisema iwapo mgonjwa atapewa tiba sahihi ndani ya saa 48, ubongo wake unaweza kurudi katika hali ya kawaida, lakini saa hizo zikizidi hawezi kupona kabisa kwa sababu maji hayo yanapomwagika ubongo hujigonga kwenye mifupa ya sakafu yake na kuharibika kabisa.


Mtaalamu wa mishipa na neva za fahamu (neurosurgeon) katika Hospitali ya Regency, Dar es Salaam, Dk Hariff Najin alisema kazi kubwa ya maji hayo ni kuulinda ubongo pindi inapotokea ajali ili usidhurike lakini endapo maji hayo yatamwagika nao huharibika.


“Haya maji yanaufanya ubongo uelee na usielemee kichwa. Hivyo inapotokea maji haya yakaisha au kupungua, ubongo hujigonga na kukosa ukinzani na kuharibika,” alisema.
Alisema maji hayo ambayo hufika hadi kwenye uti wa mgongo yakikosekana katika ubongo, husababisha damu isitembee kwenye eneo hilo jambo ambalo pia linaweza kusababisha mishipa katika sehemu ya nyuma ya ubongo kuharibiwa.
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu Muhimbili (Moi), Profesa Lawrence Museru alisema anachofahamu ni kuwa Dk Mvungi alipelekwa Afrika Kusini kwa kuwa alipata madhara makubwa kwenye ubongo na wala si kwa sababu ya kumwagika kwa maji kama ilivyoelezwa Afrika Kusini.


“Majeraha hayo yalisababisha damu kuvilia katika ubongo na kusababisha uvimbe ambao kwa kitaalamu unaitwa ‘traumatic brain injury’ na sisi tulithibitisha vipimo hivyo vya awali na kumsindikiza mpaka huko,” alisema Profesa Maseru.
Profesa Museru alisema Dk Mvungi alipata majeraha makubwa kichwani na sehemu nyingine mwilini ambayo yanaonekana yalisababishwa na kupigwa kwa vitu vyenye ncha kali au magongo na hivyo kuleta madhara katika ubongo.


Alisema hawezi kuthibitisha chanzo hasa cha kifo hicho kwani kinaweza kuwa ni kuharibika kwa ubongo au sababu nyingine zilizotokana na tatizo hilo (secondary causes).

Mwananchi

Wednesday, 13 November 2013

MUME WA ANGELA CHIBALONZA ADAIWA KUBAKA..

Katika Hali isiyokuwa ya kawaida, Mume wa Mwanamuziki nguli na Maarufu wa Muziki wa Injili, Marehemu Angela Chibalonza anayefahamika kama Elisha Muliri amedaiwa kubaka na kumpa Mimba msichana mdogo mwenye umri wa miaka 17 aliyepelekwa kanisani kwake kwa ajili ya Maombezi

Nabii Elisha Muliri na mkewe Angela Chibalonza walitikisa anga la Muziki wa Injili kwa Albamu yao ya Ebenezer na mpaka sasa ni moja ya Albamu bora sana ya Injili isiyochosha kusikiliza



Tuesday, 12 November 2013

DOKTA MVUNGI AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia hivi Punde zinasema Dokta Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba ambaye Wiki Moja na nusu iliyopita alivamiwa na Majambazi na kukatwa mapanga kichwani AMEFARIKI DUNIA


Dokta Mvungi ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu na Kiongozi mwandamizi kutoka Chama cha NCCR Mageuzi amekufa akiwa chini ya Uangalizi wa Madaktari baada ya kupata majeraha makubwa kwenye uvamizi huu ambapo ilibidi apelekwe Afrika Kusini kwa Matibabau zaidi baada ya kukaa ICU Muhimbili kwa muda wa wiki nzima bila kupata fahamu


Hili ni Pigo kubwa sana kwa Tasnia ya Elimu na Siasa nchini Tanzania


Mungu aiweke roho ya Dokta Mvungi Mahali anapostahili