Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi aliyejeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi akiwa nyumbani kwake, bado hajitambui licha ya kwamba hali yake inaendelea kuimarika.
Pia, Moi imesema kuwa majibu ya kipimo cha CT Scan alichofanyiwa Dk Mvungi katika Hospitali ya Aga Khan ni mazuri na kwamba hana tatizo lolote kubwa zaidi ya majeraha.
Dk Mvungi ambaye anaendelea kupata matibabu katika Taasisi ya Mifupa (Moi), avamiwa na kushambuliwa kwa mapanga usiku wa Jumamosi iliyopita akiwa nyumbani kwake, Kibamba Mpiji-Magoe.
Ofisa Uhusiano wa Moi,Jumaa Almasi alisema Dk Mvungi bado anaendelea kutibiwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.
Alisema hata hivyo bado hajapata fahamu tangu alipofikishwa katika taasisi hiyo.
“Hali ya Dk Mvungi inaendelea vizuri na bado anaendelea kutibiwa chini cha uangalizi wa karibu wa madaktari licha ya kwamba bado hajitambui,” alisema. Vingozi mbalimbali wa Serikali wameendelea kwenda kumuona Dk Mvungi ambapo Jumanne jioni Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye alikuwa miongoni mwa watu waliofanya hivyo.
Hadi sasa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, inawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kumshambulia Dk Mvungi kwa mapanga.
No comments:
Post a Comment