Kama wewe ni mfuatiliaji wa Muziki wa Bongo Fleva, Jina la JUX au JUX VUITTON litakuwa sio geni masikioni mwako
Ni kijana mdogo tu lakini ameweza kujipambanua kwa kutoa Nyimbo kadhaa ambazo Wakinadada wanazizimia..
Tetesi Mtaani zinasema JUX na mwanadada Jack Cliff ni wapenzi ingawa wao kila wakiulizwa huwa hawapendi kuweka wazi..Picha zao wakiwa pamoja zimezagaa Mitandao yote na zingine zikiwa kwenye Mapozi makali sana yanayobainisha hawa si marafiki wa kawaida tu..SIO ISHU
Tangu jina la JUX liingie Mtaani,kuna kitu kingine Spesheli kinachomtambulisha...KUVAA
Kama unadhani Diamond Platinumz anajua kuvaa UNAKOSEA,Mtazame kijana huyu mtanashati ambaye Mitaa imekubali kwamba kwa sasa ndiye Msanii wa Kiume aliye kwenye Tasnia ya Muziki wa Bongofleva anayejua KUNYUKA PAMBA...
Mtazame hapo chini akiwa kwenye Pozi tofauti
HAPA CHINI AKIWA NA 'DEMU WAKE' JACK CLIFF
No comments:
Post a Comment