YULE MBUNGE ALIYEOLEWA NA SERENGETI BOY AJIBU MAPIGO.ASEMA KIJANA NDIYE ALIYEFORCE NDOA
Lile sakata linaloendelea kugubika Wingu zito kwenye Vichwa vya Habari nchini kuhusu Mbunge Roswita Kasikila(60) na kijana Christian(26) limeingia kwenye Sura Mpya baada ya Mbunge huyo kujibu tuhuma zote akisema ni Kijana huyo aliyetaka ndoa.
Bwana Michael Christian amefika ofisi za gazeti moja(tunalo) kulalamika huku akionyesha Nakala ya Barua aliyomtumia Waziri wa Mambo ya Ndani,huku nakala zingine zikipelekwa kwa Mama Lwakatare na Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa.
Pichani hapo chini ni Mbunge huyo, Roswita mwenye Miaka 60
Kijana anayedai kunyang'anywa Vyeti na Mbunge huyo,Bwana Michael Christian,huyu hapa chini pichani
Mbunge huyo ameeleza kwamba ni Michael mwenyewe aliyemtongoza na kuomba wafunge ndoa huku akisema wazi Umri baina yao Sio kikwazo kwa sababu Biblia haiongelei Umri kwa wanandoa.
Akasema kwa kuwa yeye ni Mjane baada ya mumewe kufa,alijikuta akitumbukia kwenye Penzi la Kijana huyo na walifunga ndoa mwaka jana, Ndoa halali iliyofungwa Kondoa nyumbani kwa ndugu wa Michael na ilitangazwa kanisani mara 3 kinyume na ilivyoripotiwa kufungwa kwa siri na Kanisa la Mama Lwakatare
Mbunge huyo amesema hana haja ya kushikilia vyeti vya kijana huyo kwa sababu havimsaidii na amemtaka Michael kusema ukweli kwa sababu aliondoka nyumbani kwake yeye akiwa hayupo na kwa sasa anaishi na Mwanamke mwingine ambaye ni mjamzito.
Mbunge huyo amesema hana mpango wa kumshtaki kijana huyo kujibu mapigo ila ameweka wazi kwamba anao Ushahidi wa Barua Pepe zote ambazo Michael alikuwa akimtumia kumtongoza mpaka alipomkubalia na anao uwezo wa kuzitoa kama Ushahidi ikitakikana hivyo.
HAYO NDO MAMBO YA MJINI
No comments:
Post a Comment