Monday, 4 November 2013

MAREKANI YAKIRI KUPELELEZA KWA NJIA YA SIMU

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry akiri udukuzi huenda ukawa umekwenda mbali sana, haya yanajiri wakati bado mvutano unaendelea kati ya taifa hilo na mataifa ya ulaya juu ya madai ya udukuzi Baada ya siku kumi za mvutano juu ya udukuzi huo taarifa ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry ndio ya kwanza ya kukiri kuwa huenda ikawa maafisa wa Ujasusi wa Marekani wamevuka mipaka katika suala hilo la udukuzi.


Kerry pia ametetea mpango huo na kusema kwamba tangu kutokea kwa mashambulizi ya septemba 11 mwaka wa 2001 nchini Marekani, na mashambulizi mengine jijini London na Madrid, Marekani na nchi nyengine ni lazima zisimame pamoja katika kuwadhibiti magaidi ambao nia yao ni kuuwa watu na kushambulia idara za serikali.


Kerry amesema tangu mwaka huo kumekuwa na uchunguzi wa mawasiliano na kukiri kwamba uchunguzi mwengine huenda ulikuwa unavuka mipaka.Hata hivyo Kerry hakutoa maelezo yoyote juu ya tamko lake hilo, lakini akasema kwamba tukio ambalo kwa sasa linaleta mvutano na washirika wake wa karibu kama Ujerumani halitarejelewa tena.


Waziri huyo wa nchi za nje wa Marekani licha ya kukiri kwamba huenda udukuzi unaofanywa ukawa unapita mipaka pia amehakikisha kuwa hakuna mtu yoyote anayehujumiwa katika mpango huo wa kukusanya habari.


Wiki hii Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alihamaki na kumuweka sawa Rais wa Marekani Barrack Obama kuhusu madai kwamba maafisa wa Ujasusi wa Marekani wamekuwa wakichunguza mawasiliano yake ya simu na kusema kwamba iwapo hilo litathibitishwa basi hii itaondoa imani ya Ujerumani kwa Marekani.

-kibonde24-

No comments:

Post a Comment