Sunday, 3 November 2013

P'SQUARE WAFANYA KUFURU YA HELA...WAIWEKEA NAKSHI YA DHAHABU TUPU NYUMBA YAO

Kupitia Akaunti yake ya Instagram, Staa wa Kundi wa P'Square ambao tarehe 23 Mwezi huu wa November watafanya Shoo Kubwa mjini Dar es Salaam Tanzania ameonyesha Nyumba yao kubwa ambayo imenakshiwa kwa dhahabu kuanzia Sofa mpaka Vyombo vya ndani


Ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu Staa huyo amchumbie Mchumba wake rasmi kwa kumpa zawadi aina ya VOGUE EVOQUE, Model ya mwaka 2013 yenye thamani ya zaidi ya Milioni 400,Mastaa hawa wanaonekana kuishi kama WAFALME.


Kwenye Moja ya Mashairi yao waliwahi kusema,'' We are talking Money Ur talking Nonsense', wakimaanisha Pesa Inaongea,wameamua kuonyesha Jeuri ya Pesa haswa!


Tazama Picha hii ya Chini,hii ni Meza ya Chakula,Waingereza wanaita Dining Table...Kila kitu kwenye Meza hii ni DHAHABU TUPU


Picha nyingine aliyoshare Peter ni hii hapa chini..Tazama hata Midoli ni ya dhahabu...Je,Lini Rich Mavoko na Juma Nature watafikia hadhi hii??



Ikumbukwe kwamba P'Square ni wasanii Matajiri na kwenye Orodha ya Wasanii Matajiri AFRICA wanashika namba 3,wakizidiwa na AKON pamoja na Producer DON JAZZY Mwandaaji Muziki wa Lebo ya MARVIN RECORDS, Lebo iliyomtambulisha D'BANJ kwenye ulimwengu wa Muziki


Wenyewe wanakwambia WORK HARD AND PLAY HARDER....Wanafanya kazi haswa,na sasa wako kwenye TOUR ya kuizunguka Dunia wakifanya Shoo huku wakisafiri kwa PRIVATE JET wanayoimiliki.
Haondio P'SQUARE, Ndugu wawili,PETER na PAUL OKOYE

No comments:

Post a Comment