Sunday, 3 November 2013

KUMEKUCHA..HUKUMU YA MASOGANGE YAPINGWA...MAKAMANDA WA AFRIKA WAKAA KIKAO

KUMEKUCHA!


Ile Hukumu inayomhusu Dada yetu Agness Gerald au Masogange kama anavyojulikana imeonekana kuzua gumzo kubwa barani Afrika kwa Ujumla.


Kikao cha Dharura kimefanywa Mwishoni mwa Wiki iliyopita ambapo wakuu wa Vitengo vya kudhibiti Dawa za Kulevya wa nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) walikaa na kujadili na moja ya Hoja iliyozua mjadala mkubwa ni kuhusu Hukumu hii ya Masogange ambayo iliisha kimizengwe huku Faini ya Shilingi Milioni 4 ikitolewa na wao kuachiwa huru.



Sakata la Kesi hii lilianza pale ambapo Masogange na mwenzie anayefahamika kama Melisa Edward walipokamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakiwa na Mabegi yenye Kilo 150 zilizosadikiwa kuwa na Dawa Za Kulevya na wakasota kwa muda nchini Afrika Kusini ambako baadae ilidaiwa hawakuwa na Dawa bali ni Malighafi Haramu zinazoitwa EPHEDRINE


Dawa hizo zilikadiriwa kuwa na thamani ya Shilingi Bilioni 6.8 lakini baada ya muelekeo wa Kesi hiyo kuisha walilipa Faini ya kuingiza Malighafi haramu ambayo ni aidha Kifungo cha miezi 32 jela au Milioni 4.8 ambayo ililipwa na wakaachiwa huru.


Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia Madawa ya Kulevya, Kamanda Athumani Nzowa alipopigiwa Simu alisema yuko safarini Kikazi na akirudi atalitolea ufafanuzi sakata hili kwa undani

No comments:

Post a Comment